tfda_building_front.jpg

TFDA imezifutia Usajili wa Dawa tano za Binadamu kutokana na kuwepo makosa mbalimbali

 

Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano na waandishi wa habari katika kueleza maamuzi ya TFDA kufuta usajili na kubadili matumizi ya baadhi ya dawa nchini. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa TFDA Makao Mkuu


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imezifutia Usajili wa Dawa tano  za Binadamu kutokana na kuwepo makosa mbalimbali.

Hayo yameelewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mkuu   TFDA Bwana Hiiti B.Sillo  Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo alisema Mamlaka hiyo katika kupitia mifumo ya ufuatiliaji  wa usalama na ubora wa dawa nchini wamebaini uwepo wa dawa duni kwenye soko zenye madhara na zisizofaa kwa matumizi ya Binadamu.

Mkurugenzi Mkuu alieleza kuwa TFDA¬† imefikia hatua ya kufuta ¬† usajili wa aina tano za dawa za binadamu ambazo ni Dawa ya kutibu ‚ÄúFungus‚ÄĚ ya vidonge na kapsuli aina ya ketocanazole kwa sababu dawa hiyo inasababisha madhara hatarishi katika Ini kwa watumiaji.

Dawa nyingine ni ya kutibu malaria ikiwa katika mfumo wa maji na vidonge aina ya Amodiaquine inapotumika yenyewe na sababu ya kufutia usajili na kuzuia kuingia nchini ni kutokana na mabadiliko ya mwongozo wa kisera wa kupima na kutibu malaria wa mwaka 2013 uliotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, na kwamba ikitumika peke yake inaleta usugu wa vimelea vya malaria.

Bw. Sillo aliitaja dawa nyingine  ambayo ni hatari kwa matumizi ya binadamu ni Dawa ya  kutibu mafua na kikohozi ya Maji,Vidonge na Kapsuli zenye kiambato hai aina ya Phenylpropanol amine ambacho anasema kinaleta madhara hatarishi kwa binadamu kama vile kiharusi (Hemorrhagic sroke).

Mbali na hizo Dawa zengine ni Dawa ya kuua bacteria ya Sindano aina ya Chloramphenicol Sodiam Succinate inayotengenezwa nchini India pamoja na dawa ya kuua Bakteria ya Maji na kapsuli aina ya Cloxacillin ambazo zote kwa pamoja Bw. Sillo alizitaja kwamba zina madhara kwa watumiaji ikiwemo kushindwa kupumua na kupoteza Fahamu.

Katika Hatua Nyingine TFDA imebadili na kudhibiti zaidi matumizi ya aina nne za dawa nchini. Mojawapo ni Dawa ya kutibu malaria aina ya vidonge yenye mchanganyiko wa Sulphadoxine na Pyrimethamine (SP)ambayo imebadilishwa kutoka kutibu malaria na kuwa kinga ya malaria kwa kina mama wajawazito kwa mujibu wa mwongozo wa kisera wa kupima na kutibu Malaria wa mwaka 2013 wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Dawa nyingine zilizodhibitiwa zaidi ni dawa aina ya Kanamycin Amikacin na Levofloxian kwa kuruhusu dawa hizi kutumika kwa ajili ya ugonjwa wa kifua kikuu katika hospitali, vituo vya afya na zahanati pekee. Bw. Sillo alieleza sababu ya kudhibiti zaidi ni kuzuia usugu wa vimelea vya bacteria vya ugonjwa wa Kifua kikuu.

Aidha, Bwana Sillo ametoa wito kwa wamiliki wa maduka ya Dawa pamoja wananchi kuzingatia taarifa hizi za kiudhibiti kwa lengo la kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya dawa hizo. Sillo alizitaka Hospitali mbalimbali nchini pamoja maduka ya dawa kuaacha kuuza dawa hizo mara moja na kuzirudisha walikozinunua kwa ajili ya kuziteketeza.

 

 

Ziara ya Balozi wa Tanzania nchini Canada


Pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Maabara, Dkt. Adelrade Mtenga wakati wa ziara ya balozi katika ofisi za TFDA tarehe 21 Januari, 2015.

Office of the Director General

The Director General is the overall accounting officer and takes executive responsibility for strategy, operational management and service delivery of the Authority. He is responsible for the day to day operations of the organization. The office of the Director General is comprised of the Legal counsel, Internal audit and Procurement Units which provide supportive services in areas not linked to any of the specialized Directorates.

Below the Director General are the four specialized Directorates namely Directorate of Medicines and Cosmetics, Directorate of Food Safety, Directorate of Laboratory Services and Directorate of Business Support. Moreover, there are five Zone offices under Director Generals’ office located in Arusha, Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam and Dodoma regions.

Directorate of Medicines and Complementary Products

This Directorate is responsible for ensuring that all medicines, cosmetics and medical devices are correctly evaluated for quality, safety and effectiveness before being approved for use. The Directorate is also responsible for inspection and enforcement of medicines, cosmetics and medical devices. Moreover, it is responsible for control of clinical trials and adverse drug reactions monitoring and evaluation.

Directorate of Food Safety

This Directorate is responsible for ensuring safety and quality of food to be manufactured, imported, distributed or sold for human consumption.The Directorates performs food inspection services, pre-market evaluation and registration of food products and food establishments, food risk analysis, food import and export certification and food promotion control.

More Articles...

  1. Directorate of Laboratory Services
  2. Directorate of Business Development

Page 1 of 2

Events Calender

January 2015
S M T W T F S
28 29 30 31 1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31

Visitors Counter

168168
Show details

Public Education

The Authority provides unbiased information and education to the public about food, medicines, cosmetics and medical devices.

Read more: Public Education

Adverse Drug Reactions (ADRs)

Have you suffered an adverse drug reaction? If so consult your healthcare provider.

Read more: Adverse Effects

Tanzania Clinical Trial Registry

Now you can register your Clinical Trial ( i.e. Protocol Registration ) online through the Tanzania Clinical Trial Registry (TzCTR).

To access Clinical Trials Registry: Click Here!